Jumamosi, 7 Novemba 2015

NGOMA ZA ASILI


Wasanii wa Kikundi cha Ngoma za Asili cha Jembe kutoka mkoani Dodoma wakiburudisha,
 .
Baadhi ya wasanii wazee wa Kundi la Sanaa la Jivunie Tanzania wakicheza Ngoma ya Manyanga 


Wadau wa Jukwaa la Sanaa wakifuatilia burudani kutoka Kundi la Sanaa la Jivunie Tanzania.

 
Pichani  Msanii wa kundi la ngoma za asili, Juma Nkonko wa kundi la Mwenge kutoka mkoani Tabora akionyesha umahiri wa kucheza na nyoka kama alivyonaswa na kamera yetu katika fainali hizo.
  
Mpiga ngoma akipiga ngoma kwa hisia kali katika maadhimisho ya siku ya utumishi wa umma.

Mpiga ngoma akipiga ngoma kwa hisia kali.

wasichana wakisakata ngoma ya asili

wasichana wakisakata ngoma ya asili

wacheza   ngoma wakitoa burudani.

wacheza ngoma wakitoa burudani.

wacheza ngoma za asili wakiburudisha

wacheza ngoma za asili wakiburudisha
Msanii wa nyimbo zenye vionjo vya Kitanzania Batarokota.

safu ya wapiga ngoma za asili

safu ya wapiga ngoma za asili.

 Wasanii wa Ngoma za Asili kutoka Wilaya ya Sikonge, Mwanamkonko(kulia) akiongoza kuchezea Nyoka.
 Wanamuziki wa Ngoma za Asili za Maswezi wakiwa katika Onyesho. 
Wanamuziki wa Ngoma za Asili za Maswezi wakiwa katika Onyesho.
Wanamuziki wa Ngoma za Asili za Maswezi wakiwa katika Onyesho.
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mkoani Tabora wakicheza Ngoma Za Asili.
 Msanii wa Ngoma za Asili Ally Mango, akiwa kwenye Tamasha.
Wasanii wa Ngoma za Asili wakiwa katika Onyesho
 Msanii wa Ngoma za Asili Ally Mango, akiwa kwenye Tamasha.
 Msanii wa Ngoma za Asili Ally Mango, akionyesha Umahili wake katika Kucheza na Nyoka katika Onyesho.

Wasanii wa Ngoma ya Radu ya Kabila la Kinyamwezi, wakiwa katika Onyesho

 Ally Mango akionysha Jarida la wasanii.

Magufuli afanya ziara ya kushtukiza Wizara ya Fedha!


Umbali wa takribani kilomita moja kutoka ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais mpya wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli. Rais anatembea hadi Wizara ya Fedha anapowakuta ‘wazembe’ wakiwa nje ya ofisi.
Tukio hilo la jana lilikuwa la kushtukiza, lisilotarajiwa na wakazi wa jijini kumuona Rais Magufuli akiwa katika siku ya pili ya utawala wake, ‘akikatiza’ kwa mguu kwenda wizarani hapo.
Akiwa katika kampeni na baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha urais, Rais Magufuli aliwaonya watumishi wa umma kuacha kufanya kazi kwa mazoea na uzembe na wasioweza mabadiliko, waanze kuondoka.
Akiwa katika kuthibitisha kauli mbiu yake ya ‘hapa ni kazi tu’, Rais Magufuli aliingia wizarani hapo na kukuta baadhi ya viti sita vikiwa wazi, taarifa ikaeleza kwamba watumishi wahusika walikuwa nje ya ofisi kunywa chai.
Ili kupata ushahidi usiotiliwa shaka, Rais Magufuli alishika kiti kimoja baada ya kingine, akiuliza jina la mtumishi anayekitumia na mahali alipo.
Rais mpya wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amefanya ziara hiyo fupi kutoka ikulu muda mfupi baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu George Mcheche Masaju.  
Bw Masaju aliteuliwa mara ya kwanza kuwa Mwanasheria Mkuu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Januari mwaka 2015, baada ya kujiuzulu kwa George Werema.Rais  Magufuli hakuzungumza rasmi na wanahabari baada ya kumaliza ziara hiyo. 
Hata hivyo, mwandishi wa www.arcuyo.blogspot.com Paskal Linda  anasema kuna uwezekano amezungumza na maafisa wa hazina kuu kuhusu hali ya mikopo ya wanafunzi. Wakati wa kampeni, Rais John Magufuli aliahidi kufanya elimu kuwa bila malipo kuanzia shule za msingi hadi shule za sekondari. 
 
Picha juu Mwanasheria Mkuu George Mcheche Masaju.  

Taarifa kutoka ikulu ya Dar es Salaam zinasema kwenye mkutano na maafisa wakuu wa Wizara ya Fedha, Rais Magufuli aliwaagiza kuziba mianya yote inayotumiwa na wakwepa kodi. Rais Magufuli ameagiza Bunge lifunguliwe Novemba 17 na anatarajia kuwasilisha jina la Waziri Mkuu wake kwa bunge hilo Novemba 19.

Alhamisi, 5 Novemba 2015

Magufuli kuapishwa leo


Kwa mara nyingine, Tanzania itakuwa inabadilisha uongozi wake wa juu kwa amani na utulivu tangu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere aondoke madarakani kwa hiari yake mwaka 1985 baada ya kuiongoza nchi kwa miaka 23. Baada ya kung’atuka kwake, Katiba ilibadilishwa na kutoa fursa ya kuongoza kwa mihula miwili ya miaka mitano mitano kwa maana rais aliyepo anaweza kuchaguliwa tena kwa muhula wa pili.
Dk Magufuli (56) anachukua nafasi hiyo ya urais kutoka kwa Rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete ambaye anaondoka madarakani kikatiba baada ya kumaliza mihula miwili ya miaka 10. Dk Magufuli ambaye alikuwa Waziri wa Ujenzi katika Serikali ya Rais Kikwete, anaapishwa leo kuwa Rais wa Awamu ya Tano baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Jumatano, 4 Novemba 2015

Picha na matukio Kinana na Nape watembelea makumbusho ya Chifu Mkwawa


Mrithi wa Chifu Mkwawa, Abdul Adam Mkwawa akiwa amejipanga na machifu wasaidizi kumkaribisha Kinana kutembelea makumbusho ya Chifu Mkwawa katika Kijiji cha Kalenga, Iringa Vijijini wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010

Mrithi wa Chifu Mkwawa, Abdul Adam Mkwawa akiwa amejipanga na machifu wasaidizi kumkaribisha Kinana kutembelea makumbusho ya Chifu Mkwawa katika Kijiji cha Kalenga, Iringa 

Mrithi wa Chifu Mkwawa, Abdul Adam Mkwawa akitoa historia fupi ya Mkwawa kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mrithi wa Chifu Mkwawa, Abdul Adam Mkwawa akitoa historia fupi ya Mkwawa kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiishika silaha za jadi zilizotumika na Chifu Mkwawa pamoja na wasaidizi wake.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiishika silaha za jadi zilizotumika na Chifu Mkwawa pamoja na wasaidizi wake.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia picha za makabidhiano ya kichwa cha Mkwawa zilizotumika na Chifu Mkwawa pamoja na wasaidizi wake.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia picha za makabidhiano ya kichwa cha Mkwawa zilizotumika na Chifu Mkwawa pamoja na wasaidizi wake.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiishika  bunduki iliyotumiwa na Chifu Mkwawa.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiishika  bunduki iliyotumiwa na Chifu Mkwawa.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia fuvu la aliyekuwa Chifu wa Wahehe, Mkwawa alipotembelea Makumbusho ya shujaa huyo aliyepambana na wajerumani na kujiua kwa bunduki baada ya kuona yupo hatarini kukamatwa na wajerumani.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia fuvu la aliyekuwa Chifu wa Wahehe, Mkwawa alipotembelea Makumbusho ya shujaa huyo aliyepambana na Wajerumani na kujiua kwa bunduki baada ya kuona yupo hatarini kukamatwa na Wajerumani.

Kinana akiangalia makuburi ya Spika wa Bunge la Tanzania, marehemu Adam Sapi Mkwawa na mkewe ambayo ni sehemu ya kumbukumbu katika makumbusho hayo.


Kinana akiangalia makuburi ya Spika wa Bunge la Tanzania, marehemu Adam Sapi Mkwawa na mkewe ambayo ni sehemu ya kumbukumbu katika makumbusho hayo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na balozi wa shina namba moja Kalenga mjini Bi. Regina Samila na wanachama wake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na balozi wa shina namba moja Kalenga mjini Bi. Regina Samila na wanachama wake.
Vijana wa Kalenga wakiwa wamejipanga vizuri kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kwenye viwanja vya mkutano.
Vijana wa Kalenga wakiwa wamejipanga vizuri kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kwenye viwanja vya mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisimikwa uchifu wa heshima wa Kalenga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisimikwa uchifu wa heshima wa Kalenga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na machifu wa Kalenga pamoja na Viongozi wa CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na machifu wa Kalenga pamoja na Viongozi wa CCM.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kalenga.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kalenga.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu akihutubia wakazi wa Kalenga kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia wananchi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu akihutubia wakazi wa Kalenga kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia wananchi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Kalenga kwenye kichuguu ambacho Chifu Mkwawa alikuwa anahutubia watu wake
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Kalenga kwenye kichuguu ambacho Chifu Mkwawa alikuwa anahutubia watu wake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Kalenga ambapo aliwaambia kuwa Kilimo kwanza kimeleta sana faida kwa wakulima wamelima na kufanikiwa lakini tatizo linalowakabili sasa ni soko la mazao yao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Kalenga ambapo aliwaambia kuwa Kilimo kwanza kimeleta sana faida kwa wakulima wamelima na kufanikiwa lakini tatizo linalowakabili sasa ni soko la mazao yao.
Katibu Muuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wanachama waliotoka upinzani na kurudi CCM
Katibu Muuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wanachama waliotoka upinzani na kurudi CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha bendera na kofia za Chadema zilizorudishwa na wanachama waliojiunga CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha bendera na kofia za Chadema zilizorudishwa na wanachama waliojiunga CCM.
Katibu Mkuu wa CCM akikabidhi kadi kwa wanachama wapya.
Katibu Mkuu wa CCM akikabidhi kadi kwa wanachama wapya. Picha na Adam Mzee.

Jumanne, 3 Novemba 2015

JAMII YA WASUKUMA!


Pichani juu kutoka kushoto Daniel Renatus akiwa na Msanii wa mziki wa asili ya kisukuma  Paskal Linda maharufu Batarokota.

MAANA YA NENO WASUKUMA Wasukuma ni mkusanyiko wa makundi madogomadogo kutoka maeneo jirani , na kwamba kundi kubwa zaidi likiwa limetoka Kusini mwa eneo hili la mkoa wa Mwanza.Jina hili limetokana na neno sukuma maana yake wa lugha ya Kisukuma na Kinyamwezi kaskazini, yaani moja wapo wa ya pande nne za dunia yetu. Wanyamwezi ambao lugha yao inafanana sana na Kisukuma hutuita sisi tulio Kaskazini mwao "Bhasukuma" yaani watu wa kasikazini. Nasi huwaita "Bhadakama" yaani watu wa kusini.
Tangu siku zote, wasukuma na wanyamwezi walijulikana kuwa wao ni "Bhantu" na kutokana na neno hilo kumekuja kujulikana kundi linaloitwa wabantu. Kundi hili mara zote limetambulikana kwa lugha wanayozungumza ya kibantu. Hivyo, Wanyamwezi, Wakimbu hadi Wabemba walioko Zambia ni kundi kubwa la wabantu kufuatia lugha wanazozungumza.
Taarifa zingine kuhusu chimbuko la wasukuma kutoka kwenye mtandao wa internet…kwenye anwani hii.www.mwanzacommunity.com.org




Katika picha mwenye koti jeusi ndiye mzee mwenye miaka 114 ajulikanaye kama Mzee Mtalimbo. Ni mganga wa kienyeji ana wake 7 watoto 14 na wajukuu 82. Mtoto wake wa kwanza ana mika 72.



Hii ni nyumba ya mzee mtalimbo ndani pia ni maazi ya nyuki ambao ni mali yake.



Nahisi hapa ni mke na mume katika safari ya kwenda shambani. Kuwajibika kwani bila kulima hakuna kula.

Jumatatu, 2 Novemba 2015

Ijue ARCUYO

 Picha juu ni ofisi ya ARCUYO iliyopo kata ya Mkolani, jijini Mwanza barabara iendayo Shinyanga.

Kirefu cha ARCUYO ni Arts and Culture for Youths Organization, ARCUYO ni asasi isiyokuwa ya kiserikali (NGO) ambayo ilianzishwa chini ya sheria ya kanuni ya NGO No.24 ya mwaka 2002 ikiwa chini ya wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto mnamo tarehe 03/062014 na kupata usajili Na. 00NGO/00007143.
Mwalimu Hussein Kishimba akionyesha vikapu vilivyo tengenezwa kwa chelewa ambayo hutumika kuwekea vitu mbalimbali.

 ARCUYO inashungulika na vijana katika vishawishi wa kujikita na kudumisha sanaa na utamaduni ili kupitia ubunifu, vipaji, na vipawa vyao viwape fursa nahatimaye viwasaidie kujikimu kimaisha na kuwa na uwezo wa kukabiriana na changamoto zinazo wakabili.
Watoto wakijifunza kucheza ngoma za asili ya kisukuma katika kituo cha ARCUYO maeneo ya Mkolani Jijini Mwanza.
 
 Matazamio yetu ni kuona vijana wa kitanzania wanajikwamua kiuchumi, kifikra,kiafya na kielimu.Mkakati wetu kama ARCUYO ni kuhakikisha mazingira mazuri ya kiuchumi na kijamii kwa vijana yanatimizwa kama yalivyo pangwa.




Makumbusho Cultural Centre & Village Museum

Swahili class today included some wonderful singing of Tanzanian songs, both gospel and secular.  in return, the students offered a hymn or two from the Mennonite hymnal.  Also as part of Swahili class, in small groups the students were asked to act out both inappropriate and appropriate cultural behaviors.   Remember to offer and receive gifts and greetings with your right hand, avoid smelling food at a host’s house (it suggests you are unsure of the food’s quality), and please remember to greet your elders with the customary shikamoo (I offer you my respect.)
After class, we boarded daladalas from the church to visit the Makumbusho Cultural Centre & Village Museum in Dar.  The center seeks to celebrate and educate Tanzanians and visitors alike regarding the unique cultural heritage present in Tanzania’s more than 120 tribes.  More than 20 of these tribes are represented at the center through construction of houses, gardens, and industries that typify their communities in the rural landscape.   We were lucky enough to be attending during an annual 3-day celebration where villagers came to town for dancing and singing representative of their tribe.  We were also treated to a buffet of ugali, rice, vegetables, and fruit.
Tomorrow we will go to the beach for a day of respite, reading, and relaxing.  Likely Sunday, students will go to church with their families. We’ll touch base again on Monday.  Weekendi njema!  (Have a nice weekend).