Mdada akichunja pombe ya asili, na
hivyo ndivyo walivyofanya hapo kale na pia kuna baadhi ya sehemu Afrika
bado inafanyika hivyo
Na hapa ni nyumba ya asili huko Afrika ya kusini/ hasa kwa kabila la kizulu. Ambao inasemekana ni wanaukoo na wangoni.
Na hapa ni nyumba ya asili ya wangoni iliyopo Songea pale Makumbusho ya Mashujua
Ramani ya bara la Afrika
Moja ya sanaa za Kiafrika
watemi wa kisukuma wakiwa katika vazi asili la wasukuma
vijana wakisukuma wakiwa katika vazi la ngoma za kisukuma maarufu kwa jina la ngoma.
Hapa Maria Nyanjige akielezea mfano wa ngoma hii iliyotumika wakati
Chifu wa kisukuma anaoa, anasimikwa kuwa chifu au akiwa amefariki dunia
ngoma hii ilipigwa katika matukio kama hayo
Hii ni nyumba iliyohifadhi ngoma hizo zinazopigwa wakati chifu wa
kisukuma anapokuwa na matukio muhimu lakini pia ni mfano wa kiti
anachokalia chifu wa kisukuma kama unavyoiona huku chini.
Hili ni bao amalo lilitumiwa na machifu kushindana, kwa mfano wao
walikuwa hawapigi kura wakati wakichagua kiongozi wa eneo lao , ila
machifu hao walitumia bao kushindania madaraka na aliyemfunga mwenzake
kete nyingi ndiye aliyetawazwa kuwa chifu wa eneo fulani.
Hii ni ramani inayoonyesha majimbo yao ambayo machifu walitawala katika kipindi hicho.
Huu ni mwamba uliotumika kusaga nafaka mbalimbali katika familia ya
chifu na ilikuwa ni lazioma uwepo katika eneo la makazi ya chifu ikiwa
ni pamoja na Zizi la Ng”ombe, Mti mkubwa kwa ajili ya kuvuli, Mawe kwa
ajili ya kusaga dawa, ghala ya kuhifadhia nafaka kiota kikubwa kwa ajili
ya kuhifadhia kuku na sehemu maalum ya tambiko la Kisukuma
Huu ni mfano wa eneo lilitumika kwa kufanya maombi ya kimila na kufanya
toba kama kuna madhambi wamefanya, kabla ya wazungu na waarabu kuleta
dini zao.Michuzijunior mkurugenzi wa JIACHIE kushoto akiwa na Maria Nyanjige
Mhifadhi Msaidizi wa Makumbusho ya Bujora mbele ya nyumba illiyohifadhi
vifaa mbalimbali vilivyotumika kwa ajili ya michezo ya kabila la
Kisukuma Bagika na Bagalu, yaani utamaduni uliokuwa na ushindani
mkubwa kama vile Simba na Yanga.
Hii ni nyumba maalum ambayo ilitumika kuhifadhia madawa, na vifaa mbalimbali kwa ajili ya kufanyia tiba ya kiasili.
Hili ni ghala ambalo lilitumika kuhifadhia chakula na mpaka leo ghara hili hutumika katika familia
Hivi ni vifaa vilivyotumika katika shughuli za uhunzi,natumaini msomaji wa blog yangu utakua umeelewa mengi kuhusu kabila la wasukuma.
Rais Jakaya Kikwete akipiga ngoma ya kisukuma,
moja ya tamadauni za Kitanzania
Kingo, moja ya majarida ya Kitanzania.
Hapa alikuwa akitafuta Miss Tanzania wa ukweli
Ujumbe kutoka Chama cha Sanaa na Fasihi cha China
ukiangalia vinyago mjini Dar es salaam








Hivi ni vifaa vilivyotumika katika shughuli za uhunzi,natumaini msomaji wa blog yangu utakua umeelewa mengi kuhusu kabila la wasukuma.
Charles Madatta kwa niaba ya Fabian Mhoja ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Makumbusho hayo akionyesha nyumba walizokuwa wakiishi wasukuma. |
Moja ya nyumba ambazo zilikuwa zikitumia na wafalme wa Kisukuma kwa ajili ya kukutana na kucheza ngoma za asili ya kisukuma. |
noma
JibuFuta