Jumatatu, 2 Novemba 2015

Ijue ARCUYO

 Picha juu ni ofisi ya ARCUYO iliyopo kata ya Mkolani, jijini Mwanza barabara iendayo Shinyanga.

Kirefu cha ARCUYO ni Arts and Culture for Youths Organization, ARCUYO ni asasi isiyokuwa ya kiserikali (NGO) ambayo ilianzishwa chini ya sheria ya kanuni ya NGO No.24 ya mwaka 2002 ikiwa chini ya wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto mnamo tarehe 03/062014 na kupata usajili Na. 00NGO/00007143.
Mwalimu Hussein Kishimba akionyesha vikapu vilivyo tengenezwa kwa chelewa ambayo hutumika kuwekea vitu mbalimbali.

 ARCUYO inashungulika na vijana katika vishawishi wa kujikita na kudumisha sanaa na utamaduni ili kupitia ubunifu, vipaji, na vipawa vyao viwape fursa nahatimaye viwasaidie kujikimu kimaisha na kuwa na uwezo wa kukabiriana na changamoto zinazo wakabili.
Watoto wakijifunza kucheza ngoma za asili ya kisukuma katika kituo cha ARCUYO maeneo ya Mkolani Jijini Mwanza.
 
 Matazamio yetu ni kuona vijana wa kitanzania wanajikwamua kiuchumi, kifikra,kiafya na kielimu.Mkakati wetu kama ARCUYO ni kuhakikisha mazingira mazuri ya kiuchumi na kijamii kwa vijana yanatimizwa kama yalivyo pangwa.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni