Mrithi
wa Chifu Mkwawa, Abdul Adam Mkwawa akiwa amejipanga na machifu
wasaidizi kumkaribisha Kinana kutembelea makumbusho ya Chifu Mkwawa
katika Kijiji cha Kalenga, Iringa
Mrithi wa Chifu Mkwawa, Abdul Adam Mkwawa akitoa historia fupi ya Mkwawa kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiishika silaha za jadi zilizotumika na Chifu Mkwawa pamoja na wasaidizi wake.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia picha za makabidhiano
ya kichwa cha Mkwawa zilizotumika na Chifu Mkwawa pamoja na wasaidizi
wake.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia fuvu la aliyekuwa Chifu wa
Wahehe, Mkwawa alipotembelea Makumbusho ya shujaa huyo aliyepambana na
Wajerumani na kujiua kwa bunduki baada ya kuona yupo hatarini kukamatwa
na Wajerumani.
Kinana
akiangalia makuburi ya Spika wa Bunge la Tanzania, marehemu Adam Sapi
Mkwawa na mkewe ambayo ni sehemu ya kumbukumbu katika makumbusho hayo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na balozi wa shina
namba moja Kalenga mjini Bi. Regina Samila na wanachama wake.
Vijana wa Kalenga wakiwa wamejipanga vizuri kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM kwenye viwanja vya mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na machifu wa Kalenga pamoja na Viongozi wa CCM.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Iringa Ndugu Jesca Msambatavangu akihutubia wakazi wa
Kalenga kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman
Kinana kuhutubia wananchi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Kalenga
kwenye kichuguu ambacho Chifu Mkwawa alikuwa anahutubia watu wake.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Kalenga
ambapo aliwaambia kuwa Kilimo kwanza kimeleta sana faida kwa wakulima
wamelima na kufanikiwa lakini tatizo linalowakabili sasa ni soko la
mazao yao.
Katibu Muuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wanachama waliotoka upinzani na kurudi CCM.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni