Umbali wa takribani kilomita moja kutoka ofisini kwake Ikulu jijini
Dar es Salaam, Rais mpya wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli. Rais anatembea hadi Wizara ya Fedha
anapowakuta ‘wazembe’ wakiwa nje ya ofisi.
Rais mpya wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amefanya ziara hiyo fupi kutoka ikulu muda mfupi baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu George Mcheche Masaju.
Tukio hilo la jana lilikuwa la kushtukiza, lisilotarajiwa na wakazi
wa jijini kumuona Rais Magufuli akiwa katika siku ya pili ya utawala
wake, ‘akikatiza’ kwa mguu kwenda wizarani hapo.
Akiwa katika kampeni na baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha
urais, Rais Magufuli aliwaonya watumishi wa umma kuacha kufanya kazi kwa
mazoea na uzembe na wasioweza mabadiliko, waanze kuondoka.
Akiwa katika kuthibitisha kauli mbiu yake ya ‘hapa ni kazi tu’,
Rais Magufuli aliingia wizarani hapo na kukuta baadhi ya viti sita
vikiwa wazi, taarifa ikaeleza kwamba watumishi wahusika walikuwa nje ya
ofisi kunywa chai.
Ili kupata ushahidi usiotiliwa shaka, Rais Magufuli alishika kiti
kimoja baada ya kingine, akiuliza jina la mtumishi anayekitumia na
mahali alipo.
Bw Masaju aliteuliwa mara ya kwanza kuwa Mwanasheria
Mkuu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Januari mwaka 2015, baada ya
kujiuzulu kwa George Werema.Rais Magufuli hakuzungumza rasmi na wanahabari baada ya kumaliza ziara hiyo.
Hata
hivyo, mwandishi wa www.arcuyo.blogspot.com Paskal Linda anasema kuna uwezekano
amezungumza na maafisa wa hazina kuu kuhusu hali ya mikopo ya wanafunzi. Wakati wa kampeni, Rais John Magufuli aliahidi kufanya elimu kuwa bila malipo kuanzia shule za msingi hadi shule za sekondari.
Picha juu Mwanasheria Mkuu George Mcheche Masaju.
Taarifa
kutoka ikulu ya Dar es Salaam zinasema kwenye mkutano na maafisa wakuu
wa Wizara ya Fedha, Rais Magufuli aliwaagiza kuziba mianya yote
inayotumiwa na wakwepa kodi. Rais Magufuli ameagiza Bunge lifunguliwe Novemba 17 na anatarajia kuwasilisha jina la Waziri Mkuu wake kwa bunge hilo Novemba 19.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni