Historia ya Makumbusho haya inahusu vita ya Maji Maji ilivyo tokea kati
ya mwezi Julai 1905 hadi Agosti 1907. Vita hiii ilianza katika vilima
vya Umatumbi kaskazini mwa mji wa Kilwa mnamo mwezi Julai mwaka 1905.
Waanzilishi wa awali wa vita hii walikuwa ni Wamatumbi chini ya uhamasishaji wa Mganga wa jadi /Nabii aliyejulikana kwa jina la Kinjeketile Vita hii ilikuwa kama moto katika nyasi kavu na kusambaa katika makabila ya Wamwera, Wangindo, Wapogoro, Wangoni, Wabena, Wasangu na wengine. Watu hawa walipigana kupinga kukandamizwa na kulazimishwa na wakoloni wa Kijerumani namna ya kuishi, mazao ya kuzalisha na nani wa kumtumikia.
Eneo walilozikwa mashujaa hawa limekuwa eneo muhimu sana. Tukio hili lilikuwa la kuhuzunisha sana kwa watu wetu hivyo watu hawakulizungumza kwa kitambo kirefu. Baada ya uhuru (1961). Baadhi ya wazee walianzisha harakati za kuwakumbuka mashujaa hawa. Walianza kufanya maombi yao na maadhimisho katika eneo lililo karibu na eneo walilonyongwa wapiganaji hao. Shughuli hizi zilifanyika katika nyumba ya Padre Chengula.

HAPA NI PICHA YA ASKARI WA KIJERUMANI
Jina la vita vya majimaji limetokana na imani ya matumizi ya dawa iliyochanganywa
na Maji, punje za mahindi na mtama zilizosadikiwa kuwa zitampa
mpiganaji kinga ya kutodhurika kwa shambulio la risasi za majeshi ya
Wajerumani. Inakadiliwa watu 75,000 walipoteza maisha yao ukanda wa
kusini mwa Tanzania baada ya vita. Katika eneo la Ruvuma inakadiliwa
kuwa zaidi ya watu 1,000 walipoteza maisha yao.
Baada ya vita viongozi na askari walishiriki katika vita walikamatwa na
kuhukumiwa kunyongwa mpaka kufa. Tarehe 27 Februari 1907 ilikuwa siku ya
masikitiko makubwa kwa watu wa Ruvuma ambapo kadri ya watu 60
walinyongwa kwa sababu ya kushiriki katika vita. Mashujuaa hawa
walinyongwa nyuma ya eneo ambalo leo hii linajulikana kama "Songea
Club". Baada ya kunyongwa miili yao ilizikwa katika kaburi la halaiki,
lililoandaliwa na wafungwa kwa muda wa miezi miwili. Siku ya tatu
baadaye Chifu alinyongwa na kuzikwa katika kaburi lilikoandaliwa na
kaburi la halaiki.
Hapa ni kaburi la halaiki walilozikwa mashujaa wa vita ya Maji Maji, ni watu 66 walizikwa hapa.
Eneo walilozikwa mashujaa hawa limekuwa eneo muhimu sana. Tukio hili lilikuwa la kuhuzunisha sana kwa watu wetu hivyo watu hawakulizungumza kwa kitambo kirefu. Baada ya uhuru (1961). Baadhi ya wazee walianzisha harakati za kuwakumbuka mashujaa hawa. Walianza kufanya maombi yao na maadhimisho katika eneo lililo karibu na eneo walilonyongwa wapiganaji hao. Shughuli hizi zilifanyika katika nyumba ya Padre Chengula.
Wazo la kuwa na maadhimisho ya Kitaifa lilianzishwa na kamati wa wazee
wa Kingoni. Walitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa Bw. Martin Haule aliyekuwa
ameteuliwa wakati huo. Baadhi ya wazee waliokuwa katika kamati hii ni
pamoja na Xavery Zulu, Padre Chengula, Daudi Mbano, Ali Songea Mbano,
Agatha Shawa, Alana Mbawa, Mwl. Duwe, Shaibu Mkeso na Daniel Gama.
Baada ya kuwasilishwa wazo hili kwa Mheshimiwa Martin Haule, alichukua hatua za dhati katika kulishughulikia jambo hili. hatua ya kwanza ilikuwa kutambua eneo ambalo Mashujaa hawa walizikwa. eneo hili walipozikwa Mashujaa lilitambuliwa na Bw. Jumbe Darajani ambaye alishuhudia tukio la kunyongwa kwa wahenga hawa (wakati wa utoto wake). Alama iliyotumika kufahamu eneo hili ilikuwa ni mti mmoja uliojulikana kwa jina la CHIKUNGUTI. Baada ya kutambuliwa eneo hilo mheshimiwa Haule alifanya uchimbuzi na kupata baadhi ya mifupa.

Kaburi la Songea Mbano ambaye alizikwa peke yake. Na la Mji wa Songea limetokana na jina lake.
Kabla ya Bwana haule kukamilisha kazi hii alihamishiwa Mkoa wa Ruvuma
mwaka 1964. Wazo hili la kuwaenzi Wahenga hawa liliibuka tena mwaka
1979 wakati Bw Laurence Gama alipoteuliwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma.
Aliendelea na jitihada za kutekeleza wazo hili. Alianza kuhamasidha na
kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa makumbusho kwa kushirikiana na
wazee wa Ruvuma na wananchi wengine, ujenzi wa jengo la makumbusho
ulianza na kukamilika mwaka 1980.
Pamoja na kukamilisha kwa ujenzi wa jengo hili pia zilijengwa Sanamu
katika eneo la mbele ya jengo. Sanamu hizi zilijumuisha anamu ya Askari
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Mwl. J.K Nyerere na sanamu 12
zamachifu wa kingoni. Lakini kwa sasa sanamu wa hayati Mal. J.K Nyerere
imetolewa baada ya kuona haina kiwango cha juu, hivyo inaandaliwa upya
ili iweze kuwekwa upya . Kazi ya kutengeneza sanamu hizi ilifanywa na
msanii mmoja huko Arusha.
Vifaa vya awali katika makumbusho haya vilitengenezwa na Mheshimiwa
Laurence Gama, Padre Chengula na baadhi ya wazee. Vifaa vilivyokusanywa
vilijumuisha ni silaha zilizotumika wakati wa vita ya Maji Maji kama
vile:- Kwa lugha ya kingoni Chikopa (Ngao), Chibongo(Rungu), Chinjenje
(Kishoka), pia baadhi ya viti vilivyotumiwa na Chifu Mputa,vifaa vya
ndani na nguo za magome ya miti.
Kwa Hiyo kuanzia mwaka 1980 baraza la wazee lilianza kuadhimisha
maombolezo ya mashujaa walionyongwa kila ifikapo tarehe 27/2 ya kila
mwaka. Makumbusho haya yalifunguliwa rasmi tarehe 7/7/1980. Kuanzia hapo
makumbusho haya yaliendelea kutoa huduma chini ya usimamizi wa Mkoa wa
Ruvuma na wazee wanaendelea kufanya maadhimisho ya siku ya Mashujaa
katika eneo la Makumbusho haya kila mwaka.
Baadhi ya wazee ndio ambao
wamekuwa wakitoa maelezo kwa wageni wanaotembelea makumbusho haya.
Tarehe 1/9/ 2005 makumbusho haya yalikabidhiwa kwa Halmashauri ya
Manispaa ya Songea. Miaka 100 ya vita ya Maji Maji iliadhimishwa Kitaifa
katika Makumbusho haya tarehe 27/2/2006 na yalizinduliwa rasmi wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni