Pichani juu ni Mwalimu Musa Lugoyo wa shule ya sekondari Calfonia Hills ya Mkolani Mwanza, akiwa kijijini Butiama kwenye Nyumba ya makumbusho ya Mwalimu Nyerere, akianga baraza la mawaziri la mwisho la Hayati Baba wa Taifa Mwal J.K.Nyerere.
Utamaduni ni jinsi binadamu anavyokabili maisha katika mazingira yake.Neno la Kilatini lenye maana ya utamaduni ni Cultura ambalo lina usuli wake katika neno colere, linalomaanisha "kulima, kustawisha".[1]
Neno hili linafafanuliwa namna nyingi. Kwa mfano, mnamo mwaka 1952, Alfred Kroeber na Clyde Kluckhohn walikusanya orodha ya vijelezi 164 vya neno hilo katika kazi yao: Culture:a Critical Review of Concepts and Definitions.[2]
Hata hivyo, neno "utamaduni" linatumika kimsingi katika njia tatu zifuatazo:
- Maonjo ya hali ya juu katika sanaa, vilevile hujulikana kama utamaduni wa juu
- Mkusanyo wa maarifa ya binadamu, itikadi na tabia ambao hutegemea sana uwezo wa kuwasilisha mawazo na mafunzo ya kijamii kwa njia ya ishara
- Jumla ya mitazamo, kaida, malengo na maadili yanayotambulisha asasi, shirika au kikundi fulani
Katikati ya karne ya 19, wanasayansi wengine walitumia dhana ya utamaduni kurejelea uwezo wa kiubia wa binadamu.
Katika karne ya 20, "utamaduni" ulijitokeza kama dhana ya msingi katika somo la Anthropolojia. "Utamaduni" ulihusisha mambo yote ya binadamu ambayo hayakufungamana na maumbile.
Dhana ya utamaduni katika Anthropolojia ya Kimarekani ilikuwa na maana mbili: (1) Uwezo wa binadamu wa kuainisha na kuwasilisha tajiriba za kibinadamu kiishara na kutenda mambo kiubunifu; na (2) Namna mbalimbali ambazo watu wanaoishi katika sehemu mbalimbali ulimwenguni huainisha na kuwasilisha tajiriba zao za maisha na kutenda mambo kiubunifu. Kufuatia vita vya pili vya dunia, dhana hii ilipata umaarufu ingawa kwa fafanuzi tofautitofauti katika taaluma kama vile sosholojia, mafunzo ya utamaduni, saikolojia ya mipangilio na mafunzo ya usimamizi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni